Ili kuwaepusha vijana kujiunga na uhalifu na kuzama kwenye mihadarati kutokana na kukosa nafasi za kuendelea na masomo, mradi wa ujuzi wa mtaani katika eneo bunge la Mvita kaunti ya Mombasa umesaidia zaidi ya vijana 11,000 kujiunga na shule za ufundi stadi na kuwapa ujuzi wa kujikimu kimaisha. Mradi huo unawalenga vijana waliomaliza darasa la nane na kidato cha nne ambao hawawezi kuendelea na masomo kwa sababu ya umaskini.
Read MoreShirika la kijamii Mombasa limesaidia zaidi ya watu hamsini walio na akili punguani kupona na kurejea kwa hali ya kawaida. -Kupitia matibabu maalum na makao matulivu wanapopokea mafunzo ya dini, usafi na jinsi ya kurejea kwa maisha ya kawaida, wengine wameoa na wengine wakapata ajira.
Read MoreKwenye kipindi hiki cha pili, waliosaidika kutokana na hatua za shirika la kijamii Mombasa kunasua walio na akili punguani kutoka kwa hali hiyo wanashuhudia usaidizi walippokea. Kupitia matibabu maalum na makao matulivu wanapopokea mafunzo ya dini, usafi na jinsi ya kurejea kwa maisha ya kawaida, wameweza kutengamana tena na jamii na kupata ajira ilhali wengine ata wameanzisha familia jambo ambalo hawakuwa wanaweza tekeleza mbeleni.
Read MoreUtumizi wa rangi aina mbali mbali kutambulisha boda boda ya eneo tofauti Mombasa imesaidia kupunguza kesi za uhalifu zinazohusiana na sekta hiyo.Ili kutofautisha wanabodaboda na raia ambao wanatumia piki piki kama njia ya usafiri na kusababisha uhalifu, rangi linapakwa kwenye bamba lenye nambari ya usajili pamoja na nambari mwafaka ya kujitambulisha ambayo inaonyesha pia eneo.
Read MoreKilimo kimesaidia sana kumaliza unyanyapaa na kutengwa kwa watu wanaouguwa ugonjwa wa ukimwi kaunti ya Kakamega. Baada ya vikundi vya watu wanaouguwa ugonjwa huo kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa. Sasa wanapata mazao ambayo huuzia jamii na kwa kufanya hivyo wanakuwa na ukaribu nao.
Read MoreKupitia mradi wa "Tuwajali Wajane" zaidi ya wajane 800 wamefunzwa na kuwezeshwa kujitegemea kifedha. Wanapata ushauri nasaha, mafunzo ya kibiashara na pia kuunganishwa na hazina za wanawake ambayo wanapewa mikopo ya biashara.
Read MoreUhamasisho wa wakaaji wa Mbeere Kusini dhidi ya kuwachisha wanafunzi shule ili wasaidie katika kilimo na biashara ya miraa inazaa matunda. Kupitia mikutano za hadhara ambazo zinaandaliwa mara mbili kwa mwezi na idara ya utawala katika vijiji kupitia machifu na manaibu wao, wananchi wamekuwa wakielimishwa na kuhimizwa kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto na madhara ya kuwahusisha katika shughuli za miraa.
Read MoreUkosefu wa maji katika wadi la Makima ilikuwa inalazimisha wakaazi kwenda masafa marefu kama kilomita tano kuyatafuta. Mmoja wapo wa hatari wa safari iyo ilikuwa kuliwa na mamba ambao walikuwa wanapatikana kwenye bwawa la maji. Lakini mradi wa kuleta maji karibu na wakaazi kupitia kuweka matangi katika soko mbali mbali yameondoa tatizo la maji na hatari iyo ya mamba.
Read MoreWakulima wa maembe katika Kaunti ya Makueni wamesaidika kupunguza hasara baada ya Serikali ya kaunti kuweka mbinu mbali mbali ili kuwaepusha na hasara hizo zilizoletwa na ukosefu wa soko na mazao kuliwa na wadudu waharibifu. Kwa kuwaundia kiwanda cha kusagia maembe na kuwaelimisha jinsi ya kutumia mitego badala ya kemikali ili kunasa wadudu waharibifu, wakulima wa maembe wameweza kupanua soko yao na kufikia hadi soko za kigeni.
Read MoreMbinu mbalimbali za kiafya zilitumika kuzuia kusambaa kwa mbu anayesababisha homa ya chikungunya kutoka kaunti ya Mombasa hadi kaunti jirani ya Kilifi.Hamasa hizo zilitolewa na wahudumu wa afya wa nyanjani wa kujitolea katika gatuzi ndogo 4 za Rabai.Ambapo wahudumu walizungukia nyumba kuhakikisha kuwa mazingira ni safi na kwamba hakuna maeneo ya mbu kuzaana.
Read MoreCollections are versatile, powerful and simple to create. From a customized course reader to an action-guide for an upcoming service-learning trip, collections illuminate themes, guide inquiry, and provide context for how people around the worls are responding to social challenges.
Name and describe your collection
Add Stories
Add external links at any time
Add to your collection over time and share!
Successfully added!