Kilimo kimesaidia sana kumaliza unyanyapaa na kutengwa kwa watu wanaouguwa ugonjwa wa ukimwi kaunti ya Kakamega. Baada ya vikundi vya watu wanaouguwa ugonjwa huo kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa. Sasa wanapata mazao ambayo huuzia jamii na kwa kufanya hivyo wanakuwa na ukaribu nao.
Read MoreMbinu mbalimbali za kiafya zilitumika kuzuia kusambaa kwa mbu anayesababisha homa ya chikungunya kutoka kaunti ya Mombasa hadi kaunti jirani ya Kilifi.Hamasa hizo zilitolewa na wahudumu wa afya wa nyanjani wa kujitolea katika gatuzi ndogo 4 za Rabai.Ambapo wahudumu walizungukia nyumba kuhakikisha kuwa mazingira ni safi na kwamba hakuna maeneo ya mbu kuzaana.
Read MoreKaunti ya kisumu na shirika la kijamii la Kidogo limejenga kituo cha kina mama kuingia na kunyonyesha watoto wao katika soko la Kibuye. Kituo hicho kinatoa mazingira mazuri na tulivu ya kina mama kunyonyesha watoto wao. Mama anapofika katika kituo hicho, kuna mhudumu wa afya anayeshika mtoto ili mama aoshe mikono, kisha apewe kiti akae anyonyeshe mtoto. Pia kuna jokovu la kuhifadhi maziwa ya mama kwa walio na maziwa mengi na wengetaka kukamua.
Read MoreUjio wa ugatuzi umepunguza changamoto zinazoandamana na safari za mbali kutafta huduma za afya katika Kaunti ya Kwale. Kupitia mfumo hii, serikali ya kaunti imeweza kutenga fedha za kujenga zaid ya vituo vya afya 37 katika maeneo mbali mbali na kurahisisha jinsi wakaaji wanapata huduma za afya. Vituo hivyo vinapeana huduma mbali mbali za afya ikiwemo huduma za kujifungua, madawa na maabara na kadhalika.
Read MoreDawa za tiba kinga zinasaidia kupunguza madhara ya ugonjwa wa kichocho katika kizazi kipya maeneo ya Lake zone nchini Tanzania. Serikali inakinga watoto kutokana na madhara za ugonjwa huu kupitia mradi wa kupeana dawa za Prazequantel na albendazole bure katika shule za msingi na zahanati. Licha ya haya, wanafunzi pia wanapewa maji safi ya kunywa mashuleni ili kuwaepusha na maambukizo mapya.
Read MoreKabla ya mwaka wa 2008, madaktari wa Tanzania hawakuwa wanafanya upasuaji wa moyo lakini baada ya kupata mafunzo kutoka India na Israel, wamepata ujuzi wa kuokoa maisha. Ujuzi huo umefanya kuzinduliwa kwa taasisi ya Jakaya Kikwete ambayo imebobea kwenye huduma za moyo huku wakiweza kushughulikia zaidi ya kesi 800 kwa mwaka.
Read MoreSerikali ya Tanzania ilipeleka madaktari nchini India kupata mafunzo ili kukabiliana na ukosefu wa huduma za matibabu ya kibingwa hasa kwa magonjwa ya moyo. Juhudi hili limeweza kuchangia kuzalishwa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambayo huhudumia takribani wagonjwa 800 kila mwaka.
Read MoreTiba kwa mbali umesaidia kukabiliana na uchache wa madaktari wa kitaalamu na kuimarisha sekta ya afya katika kaunti ya Makueni. Kupitia mfumo huo, wakaazi wameweza kupata huduma za kitaalamu ata katika hospitali za nyanjani na kuwapunguzia gharama ya kufunga safari za mbali ili kupata huduma hizo.
Read MoreIli kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu, zaidi ya kuhimiza wakaaji kujenga choo, kaunti ya Embu pia inaelimisha wanakijiji kutumia choo na kukuwa wasafi kupitia wanafunzi, viongozi wa vijiji na madaktari wa nyanjani. Kupitia mbinu hizi idara ya afya imeweza kupunguza kesi za kipindupindu.
Read MoreUchimbaji wa vyoo na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga na kutumia vyoo kumesaidia kuangamiza ugonjwa wa kipindupindu kaunti ya Embu.Idara ya afya inatumia madaktari wa nyanjani wakujitolea kuelemisha watu umuhimu wa kujenga na kutumia choo kwa njia nzuri.Wanahakikisha kuwa kila boma limejenga angalau choo kimoja.
Read MoreCollections are versatile, powerful and simple to create. From a customized course reader to an action-guide for an upcoming service-learning trip, collections illuminate themes, guide inquiry, and provide context for how people around the worls are responding to social challenges.
Name and describe your collection
Add Stories
Add external links at any time
Add to your collection over time and share!
Successfully added!