Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yamejitolea kuwainua kimaisha na kuwafunza ukulima vikundi vya watu wanaouguwa ugonjwa wa ukimwi kaunti ya Kakamega.Hii ni baada ya waathiriwa hao kuja pamoja kutiana moyo baada ya kuhisi kutengwa na jamii.Mashirika hayo yanawafunza mbinu za kisasa za ukulima zinazowapatia mazao ambayo wanaweza kuuza na kupata pesa za kujikimu kimaisha.
Read MoreUhamasisho wa wakaaji wa Mbeere Kusini dhidi ya kuwachisha wanafunzi shule ili wasaidie katika kilimo na biashara ya miraa inazaa matunda. Kupitia mikutano za hadhara ambazo zinaandaliwa mara mbili kwa mwezi na idara ya utawala katika vijiji kupitia machifu na manaibu wao, wananchi wamekuwa wakielimishwa na kuhimizwa kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto na madhara ya kuwahusisha katika shughuli za miraa.
Read MoreWakulima wa maembe katika Kaunti ya Makueni wamesaidika kupunguza hasara baada ya Serikali ya kaunti kuweka mbinu mbali mbali ili kuwaepusha na hasara hizo zilizoletwa na ukosefu wa soko na mazao kuliwa na wadudu waharibifu. Kwa kuwaundia kiwanda cha kusagia maembe na kuwaelimisha jinsi ya kutumia mitego badala ya kemikali ili kunasa wadudu waharibifu, wakulima wa maembe wameweza kupanua soko yao na kufikia hadi soko za kigeni.
Read MoreMbinu mbalimbali za kiafya zilitumika kuzuia kusambaa kwa mbu anayesababisha homa ya chikungunya kutoka kaunti ya Mombasa hadi kaunti jirani ya Kilifi.Hamasa hizo zilitolewa na wahudumu wa afya wa nyanjani wa kujitolea katika gatuzi ndogo 4 za Rabai.Ambapo wahudumu walizungukia nyumba kuhakikisha kuwa mazingira ni safi na kwamba hakuna maeneo ya mbu kuzaana.
Read MoreKufuatia mkurupuko wa homa ya Chikungunya kaunti ya Mombasa, serikali ya kaunti iliweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na mkurupuko huo. Ikiwa ni pamoja na utumizi wa magari ya kupuliza dawa kuua mbu.Magari 5 yalitumiwa katika zoezi hilo ambapo yalizunguka maeneo bunge yote 6 kaunti ya moja kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Read MoreUtumizi wa plastiki kujenga nyumba ya vifaranga kaunti ya Bungoma inatunza mazingira pamoja na kupunguza gharama ya kujenga nyumba hizo. Kwa kutumia mabaki ya plastiki hususan mtungi za mafuta ya kupika, wafugaji wa kuku wanajenga sanduku zinazotumika kama nyumba ya kufuga vifaranga wa siku moja hadi mwezi mmoja.
Read MoreKaunti ya kisumu na shirika la kijamii la Kidogo limejenga kituo cha kina mama kuingia na kunyonyesha watoto wao katika soko la Kibuye. Kituo hicho kinatoa mazingira mazuri na tulivu ya kina mama kunyonyesha watoto wao. Mama anapofika katika kituo hicho, kuna mhudumu wa afya anayeshika mtoto ili mama aoshe mikono, kisha apewe kiti akae anyonyeshe mtoto. Pia kuna jokovu la kuhifadhi maziwa ya mama kwa walio na maziwa mengi na wengetaka kukamua.
Read MoreUjio wa ugatuzi umepunguza changamoto zinazoandamana na safari za mbali kutafta huduma za afya katika Kaunti ya Kwale. Kupitia mfumo hii, serikali ya kaunti imeweza kutenga fedha za kujenga zaid ya vituo vya afya 37 katika maeneo mbali mbali na kurahisisha jinsi wakaaji wanapata huduma za afya. Vituo hivyo vinapeana huduma mbali mbali za afya ikiwemo huduma za kujifungua, madawa na maabara na kadhalika.
Read MoreSinge’nge inayotengenezwa kwa mabati madogo madogo ambayo hufungwa kwa kamba na kuzungushwa katika mpaka wa shamba imesaidia kupunguza mzozo kati ya wanyamapori na binadamu katika kaunti ya Taita Taveta. Mabati hayo madogo yanapogongana hutoa sauti inayotishia ndovu na wakati wa usiku mabati hayo yanang’aa kiasi cha kuwatishia ndovu wasifikie mashamba hayo.
Read MoreDawa za tiba kinga zinasaidia kupunguza madhara ya ugonjwa wa kichocho katika kizazi kipya maeneo ya Lake zone nchini Tanzania. Serikali inakinga watoto kutokana na madhara za ugonjwa huu kupitia mradi wa kupeana dawa za Prazequantel na albendazole bure katika shule za msingi na zahanati. Licha ya haya, wanafunzi pia wanapewa maji safi ya kunywa mashuleni ili kuwaepusha na maambukizo mapya.
Read MoreCollections are versatile, powerful and simple to create. From a customized course reader to an action-guide for an upcoming service-learning trip, collections illuminate themes, guide inquiry, and provide context for how people around the worls are responding to social challenges.
Name and describe your collection
Add Stories
Add external links at any time
Add to your collection over time and share!
Successfully added!